MAHAKAMA YATUPILIA MBALI KESI INAYOPINGA UTEUZI WA NOORDIN HAJI
Mahakama Kuu imetupilia mbali ombi lililokuwa likipinga kuteuliwa kwa Noordin Haji kama Mkurugenzi wa Huduma ya Kitaifa ya Ujasusi (NIS) iKisema kuwa uamuzi wa Rais katika kuwateua maafisa wakuu wa umma ni wa hiari yake na unalindwa na Katiba.
Katika uamuzi wake, mahakama iMEbainisha kuwa hoja za waliowasilisha kesi hiyo kwamba Haji hakupaswa kuteuliwa kutokana na kuwepo kwa kesi nyingine katika Mahakama Kuu na Tume ya Huduma za Umma hazikuwa na msingi wa kisheria.
Mahakama pia iMEsema kuwa mahakama inaweza kuingilia uteuzi huo tu iwapo Rais atakiuka Katiba, na kwamba kuingilia mchakato huo bila sababu za kikatiba kungekuwa kuvuka mipaka ya mamlaka ya mahakama.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 




























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































