WABUNGE WA MLIMA KENYA WAMKINGIA KIFUA KINDIKI
Wabunge kutoka eneo la Mlima Kenya upande wa Kenya Kwanza wamesisitiza kuwa hawatakubali mazungumzo yoyote ya kumuunga mkono Rais William Ruto katika azma yake ya urais mwaka 2027 iwapo Naibu wa Rais Kithure Kindiki hataendelea kushikilia nafasi hiyo katika uchaguzi ujao.
Viongozi hao wameeleza kuwa hawakubaliani na kauli ya chama cha ODM inayodai kupewa nafasi hiyo katika mazungumzo ya kuungana na UDA kwa lengo la kumuunga mkono Ruto.
Aidha Wamesema msimamo wao ni kuhakikisha maslahi ya eneo hilo yanalindwa kabla ya kuingia katika makubaliano yoyote ya kisiasa kuelekea uchaguzi mkuu wa 2027.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 



































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































