#Football #Sports

HARAMBEE STARLETS WAIMARISHA MAANDALIZI

Timu ya taifa ya soka ya wanawake Harambee Starlets inajiandaa kwa mkondo wa marudiano wa mechi ya kufuzu katika mashindano ya ubingwa wa wanawake bara Afrika WAFCON dhidi ya Gambia hapo kesho.

Starlets wataingia kwenye mechi hiyo wakihitaji angalau sare ya aina yoyote ili kufuzu, baada ya kupata ushindi wa mabao 3:1 katika mkondo wa kwanza ugani Nyayo Ijumaa iliyopita.

Mechi hiyo itasakatwa katika uwanja wa Stade Lat Dior nchini Senegal kutokana na Gambia kukosa uwanja ulioafikia viwango hitajika vya CAF.

Tayari vipusa hao wanaonolewa na kocha Beldine Odemba wamo nchini Senegal kwa maandalizi, na ushindi utawahhakikishia sio tu tiketi ya kuingia WAFCON, bali shilingi milioni 1 kwa kila mchezaji kutoka kwa Rais William Ruto.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

HARAMBEE STARLETS WAIMARISHA MAANDALIZI

WETANG’ULA ATETEA SHERIA YA KOMPYUTA

HARAMBEE STARLETS WAIMARISHA MAANDALIZI

NAIROBI UNITED WAANDIKISHA TAARIFA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *