JUNIOR STARS WAJIANDAA KUIVAA ETHIOPIA
Kocha wa timu ya taifa kwa wachezaji wasiozidi umri wa miaka 17 William Muluhya, amesema kikosi chake kitatumia ushindi mara 2 katika mechi za awali kama motisha kwenye mechi yao ya mwisho ya makundi dhidi ya Ethiopia hii leo.
Licha ya timu zote 2 kufuzu awamu ya semifainali, Stars wanalenga kutwaa ubingwa wa michuano ya CECAFA, na watahitaji kuwatungia wenyeji sheria kwenye mchuano huo uliokuwa umeratibiwa kusakatwa hapo kesho.
Timu 2 bora kwenye mashindano hayo ya CECAFA zitafuzu kusakata dimba la mataifa bingwa barani Afrika AFCON kwa wachezaji wasiozidi umri wa miaka 17.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































