#Local News

MFUMO MPYA WA FAINI ZA TRAFIKI WA NTSA WAPINGWA

Ombi limewasilishwa mahakamani kupinga mfumo mpya wa NTSA wa utoaji wa faini za papo kwa hapo kwa wanaokiuka sheria za trafiki, huku likitaka utekelezaji wake usimamishwe mara moja.

Ombi hilo lililowasilishwa na Kennedy Maingi Mutwiri linajiri baada ya NTSA kutangaza kuwa mfumo huo mpya wa usimamizi wa faini za trafiki umeanza kutumika.

Mlalamishi anadai mfumo huo hauna msingi wa kisheria na unakiuka haki za kikatiba, akisema makosa ya trafiki chini ya Sheria ya Trafiki yanapaswa kusikilizwa mahakamani ili mshtakiwa apewe nafasi ya kujitetea na kupinga ushahidi.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *