#Athletics #Sports

SAWE KUTETEA UBINGWA WAKE LONDON

Bingwa mtetezi wa mbio za London Marathon Sabastian Sawe, ameratibiwa kutetea ubingwa wake katika mbio zitakazoandaliwa tarehe 26 Aprili, akiamini kuwa huenda akahitaji kuvunja rekodi aliyoandikisha ili atetee ubingwa wake kutokana na ushindani mkali.

Mkenya huyo mwenye umri wa miaka 29, anatarajia ushindani kutoka kwa vigogo wenza akiwemo Jacob Kiplimo wa Uganda aliyemaliza wa pili katika mbio za mwaka jana, na ambaye ameshinda mataji 3 mfululizo ya mbio za Cross Country, rekodi ya dunia ya half marathon na ushindi katika mbio za Chicago Marathon.

Sawe ameliambia shirika la habari la Reuters kwamba alijivunia kushiriki mbio za London Marathon, ambayo ilikuwa ni mara yake ya kwanza, akikariri haja ya juhudi zaidi kama vile za mwendazake Kelvin Kiptum ili kutetea ubingwa wake.

Kiptum aliweka rekodi ya 2:01:25 mnamo mwaka 2023, ila Sawe aliibuka mshindi kwa muda wa 2:02:27 ingawa hakuvunja rekodi ya Kiptum.

Wengine wanaotarajiwa ulingoni katika safu ya wanaume ni bingwa wa 2024 Olympic katika mbio za mita 10,000, Mganda Joshua Cheptegei, bingwa wa Olympic Marathon Tamirat Tola wa Ethiopia na mwenzake Yomif Kejelcha, na Mjerumani Amanal Petros aliyekosa nishani ya dhahabu kwa sekunde 3 pekee katika ubingwa wa mwaka jana.

Safu ya akina dada inajumuisha bingwa mtetezi Tigst Assefa wa Ethiopia, bingwa wa dunia Peres Jepchirchir wa Kenya na bingwa wa Olimpiki Sifan Hassan wa Uholanzi.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

SAWE KUTETEA UBINGWA WAKE LONDON

RUTO AWATAKA VIJANA KUKUMBATIA NYOTA

SAWE KUTETEA UBINGWA WAKE LONDON

NAIBOIS KUANZA UTETEZI DHIDI LA L15 FC

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *