WAWILI WAUAWA KWA KUPIGWA RISASI KAKAMEGA
Watu wawili wamepoteza maisha kwa kupigwa risasi, huku mtu wa tatu akiendelea kupokea matibabu hospitalini akiwa na majeraha mabaya ya risasi, kufuatia makabiliano kati ya wakazi wa kijiji cha Mukulusu na maafisa wa Huduma ya Misitu ya Kenya katika eneo la Shinyalu, Kaunti ya Kakamega.
Vurugu hizo zilianza baada ya mzozo kuzuka kuhusu njia ambayo lori lililokuwa limebeba mchanga wa ujenzi lilipaswa kupita likitoka katika kituo cha kuhifadhi mchanga.
Akithibitisha tukio hilo, Kamanda wa polisi wa kaunti ndogo ya Shinyalu, Daniel Mukumbu, amesema maafisa hao walijilinda baada ya kushambuliwa na wenyeji.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 



































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































