FKF YAINGIA MOU KUINUA SOKA YA VIJANA
Shirikisho la Soka nchini FKF limeingia makubaliano ya ushirikiano na chuo cha mafunzo ya soka cha Acakoro Football Academy na kuzindua mfumo wa kwanza nchini wa hali ya juu unaotoa makazi kwa wachezaji kwa ajililumu kwa ajili ya kukuza timu ya taifa ya vijana.
Ushirikiano huo unalenga kushughulikia mapungufu ya muda mrefu katika uendeshaji wa soka ya vijana kwa kuanzisha njia ya pamoja na ya muda mrefu ya kuwakuza wachezaji chipukizi kutoka maeneo mbalimbali ya nchi. Kuanzia mwezi huu, FKF na Acakoro watafanya mchujo wa pamoja wa wachezaji bora waliozaliwa mwaka 2011 katika kanda tano, ambapo wanaofanya vizuri zaidi watapata ufadhili kamili kujiunga na mpango wa bweni katika kituo cha ekari 25 cha Acakoro kilichoko Homa Bay.
Mpango huo unajumuisha elimu inayoendana na CBC, mafunzo ya kisasa ya soka, sayansi ya michezo, uchambuzi wa kiufundi, pamoja na maendeleo ya kina ya kibinafsi, ikitoa mazingira yanayofikia viwango vya kimataifa. Wachezaji watakaochaguliwa wataingizwa moja kwa moja katika mchakato wa timu za taifa za vijana za FKF kuanzia U15 hadi U17, na hivyo kuunda msingi wa kikosi kitakachojiandaa kuelekea Kombe la Dunia la FIFA U17 mwaka 2027 nchini Qatar.
Rais wa FKF, Hussein Mohammed, alisema ushirikiano huu unaonyesha dhamira ya shirikisho kuimarisha miundo ya soka ya vijana.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































