LIGI YA KPL YAINGIA WIKI YA 21
Ligi kuu ya soka nchini, KPL, inaingia wiki ya 21 wikendi hii huku viongozi Gor Mahia wakishikilia Kikiki usukani wa ligi hiyo wakilenga ubingwa wa 22.
Green Commandos wanaongoza ligi hiyo na pointi 43 baada ya kusakata mechi 20, wakifuatiwa na mahasimu wao AFC Leopards walio na pointi 37 ingawa wana mechi moja mkononi, nao Shabana FC wakishikilia nafasi ya tatu kwa pointi 34.
Kakamega Homeboyz walio katika nafasi ya 5, wataialika Sofapaka leo saa saba adhuhuri kwenye mechi ya kwanza ya wikendi hii.
Kesho, mechi kadhaa zimeratibiwa kusakatwa ambapo Nairobi United watalenga kujisahaulisha masaibu ya dimba la mashirikisho barani Afrika watakapomenyana na Bidco United, nao AFC Leopards watoe kucha zao dhidi ya barua za Posta Rangers.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 




























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































