#Football #Sports

CARRICK AENDELEZA REKODI MURWA

Meneja mshikilizi wa Manchester United, Michael Carrick, aliendeleza rekodi yake ya ushindi, tangu kuchukua hatamu za klabu hiyo kutoka kwa Ruben Amorim, sasa akiwa na ushindi katika mechi 3 mfululizo.

Bao la Benjamin Sesko katika dakika za majeruhi zilizima uasi wa Fulham waliotishia kuwapokonya United alama, na kuishia katika ushindi wa mabao 3-2.

United walichukua uongozi kupitia kwa Casemiro, kabla ya Matheus Cunha kuongeza uongozi.

Hata hivyo, mambo yalibadilika wakati Raul Jimenez alipachika wavuni mkwaju wa penalti kabla ya Kevin kuisawazishia Fulham.

Ushindi wa United umewaweka katika nafasi ya 4 kwa pointi 41, 12 pekee nyuma ya viongozi Arsenal walioandikisha ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Leeds.

Manchester City na Aston Villa waliiondolea Arsenal shinikizo baada ya kukosa ushindi.

City walipoteza uongozi wa mabao 2-0 na kutoka sare ya mabao 2-2 ugenini dhidi ya Tottenham, huku Astin Villa wakipigwa nyumbani na Brentford bao 1-0.

City wanaifuata Arsenal kwa pointi 6.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

CARRICK AENDELEZA REKODI MURWA

MIGORI YOUTH WASALIA KWENYE USAKANI NSL

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *