#Football #Sports

CITY WAIKARIBIA ARSENAL

Mshambulizi wa Manchester City Erling Haaland alivunja rekodi ya Alan Shearer na kuwa mchezaji wa kasi zaidi kufikisha magoli 100 katika ligi kuu ya Uingereza, usiku ulioshuhudia City wakiweka shinikizo kwa viongozi wa ligi Arsenal wakipunguza pengo la pointi kufuatia ushindi wa mabao 5-4 dhidi ya Fulham.

Raia huyo wa Norway alifunga bao lake la kihistoria katika dakika ya 17 kutokana na krosi ya Jeremy Doku, na kufikisha magoli 100 katika mechi 111, tofauti na Shearer ambaye alifanya hivyo katika mechi 124.

Bao hilo aidha lilitamatisha kiangazi cha magoli kwa Haaland, ambaye alikuwa amecheza mechi 3 mfululizo bila kufunga, sasa akiongoza kwa ufungaji wa mabao, akiwa na 15 katika mechi 14 za ligi kuu EPL.

Phil Foden alifunga mara 2, huku kiungo Tijan Reijnders akifunga moja na kiungo mkabaji wa Fulham Sander Berge akijifunga.

Hata hivyo, hofu kwa meneja Pep Guardiola itakuwa kuhusiana na jinsi vijana wake walivyoporomoka katika kipindi cha pili, Fulham walipotoka mabao 5-1 chini na kufunga mabao 3, mechi ikiisha kwa mabao 5-4.

Mechi zaidi zitachezwa hii leo ambapo vigogo Arsenal watalenga kurejesha uongozi wa pointi 5 watakapoialika Brentford.

Leeds wataikaribisha Chelsea, Burnley wamenyane na Crystal Palace nao Wolves wakilenga kuvamia msitu wa Nottingham Forest.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

CITY WAIKARIBIA ARSENAL

KENYA TAYARI KUWAKILISHA U-21 TAEKWONDO

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *