VIJANA WEBUYE WAHIMIZWA KUCHUKUA KURA
Wakazi wa eneo bunge la Webuye West wametakiwa kujitokeza kwa wingi kusajiliwa katika zoezi linaloendelea la upigaji kura, idadi ndogo ikiripotiwa kufikia sasa.
Kwa mujibu wa afisa wa tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC eneo hilo Bernard Mutali, huenda hali hiyo imechangiwa na umbali wa kituo ambako usajili huo unafanyika.
Wakati uo huo, makundi ya vijana eneo hilo yakiongozwa na Anthony Nyongesa, yameanzisha harakati za kuwahamasisha vijana kujisajili.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 


























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































