#Football #Sports

MOYES AMTETEA JACK GREALISH BAADA YA USHINDI DHIDI YABOURNEMOUTH

Kocha wa Everton, David Moyes, amesisitiza kuwa Jack Grealish
hajakuwa mchezaji wa kukatisha tamaa, baada ya winga huyo

kufunga bao lake la pili msimu huu na kusaidia The Toffees kushinda
1-0 dhidi ya Bournemouth,

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30, ambaye alipoteza nafasi
yake kwa Pep Guardiola msimu uliopita, alikuwa amefunga bao moja
pekee katika mechi zake 14 za kwanza akiwa Everton kabla ya kutupia
bao la ushindi dhidi ya Bournemouth.

Moyes amesema Grealish bado ana thamani kubwa katika kikosi,
akiongeza kuwa anafurahia kurejea kwa kiwango na uwezo wake
uwanjani.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *