FAMILIA ZAIDI YA ELFU TATU ZAKABILIWA NA HATARI YA MAFURIKO
Familia zaidi ya elfu tatu katika kaunti nane za eneo la kati ziko katika hatari ya kukumbwa na mafuriko pamoja na maporomoko ya ardhi kufuatia mvua kubwa inayoendelea kunyesha.
Kwa mujibu wa Shirika la Msalaba Mwekundu Kenya, tayari familia 48 zimeathirika msimu huu wa mvua huku shirika hilo likitoa wito kwa wakazi kuhama mapema kuelekea maeneo ya juu kwa usalama wao.
Shirika hilo la kibinadamu linaonya kuwa maji ya mafuriko ni hatari zaidi kuliko yanavyoonekana na kuwataka wakazi kuchukua tahadhari ili kuepuka madhara yanayoweza kujitokeza
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 














































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































