KAULI YA RUTH ODINGA KUHUSU USHIRIKIANO WA ODM-UDA
Bado ni mapema kwa chama cha ODM kuingia kwenye makataba wa kisiasa na UDA kuelekea uchaguzi mkuu ujao, ikizingatiwa kuwa ajenda 10 zilizoafikiwa kati ya Rais William Ruto na kinara mwanzilishi wa ODM marehemu Raila Odinga hazijatekelezwa.
Haya ni kulingana na Ruth Odinga, ambaye ni mwakilishi wa kike wa kaunti ya Kisumu na dadake Odinga, anayetaka ODM kujipanga upya kabla ya kuafikia makubaliano yoyote ya kisiasa.
Kulingana naye, hakuna sababu za makubaliano mapya kabla ya utekelezaji wa ajenda hizo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 


































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































