SALLY BOLO:KIPIGO CHA GOR MAHIA MWAMKO WA KOGALO
Makamu wa rais wa Gor Mahia, Sally Bolo amesema kuwa kushindwa kwa mechi ya 98 ya mashemeji derby dhidi ya wapinzani wao AFCleopards, ni mwamko wa k’ogalo katika ligi kuu ya kenya.
Kipigo cha gor mahia cha 1-0 dhidi ya ingwe kilimaanisha k’ogalo wameshindwa kushinda katika mashemeji derby katika makala matatu mfululizo, baada ya kushiriki viporo nyumbani na ugenini msimu uliopita. Kufuatia onyesho kuu la vijana wa Fred Ambani Bolo amekubali kushindwa na kukiri kwamba kocha Charles Akonnor na wasaidizi wake wanapaswa kujifunza kutokana na kipigo hicho.
Imetayarishwa na Jones Koikai
English 







































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































