MATIANG’I ASHINIKIZA MAGEUZI YA ELIMU
Aliyekuwa Waziri wa usalama Fred Matiang’i, amehimiza haja ya vikao vya dharura kuandaliwa ili kujadili na kupata suluhu kwa changamoto zinazoikabili sekta ya elimu nchini.
Akizungumza kwenye kaunti ya Kiambu, Matiang’i ambaye ni naibu kinara wa chama cha Jubilee, amesisitiza haja ya sekta hiyo kufanyiwa mageuzi ili kuilainisha.
Aidha, amekosoa madai kwamba serikali imeingiza siasa katika utoaji wa vitambulisho vya kitaifa kwa raia wa kigeni.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































