POLICE FC WAFYATUA UPYA
Kocha mkuu wa Police FC Dusan Stonajovic amesifu ari ya wachezaji wake baada ya kuiongoza timu hiyo kupata ushindi wa bao 1:0 dhidi ya Sofapaka kwenye mechi yake ya kwanza tangu alipotambulishwa rasmi kuwaongoza mabingwa hao
Mshambuliaji wa zamani wa Sofapaka Edward Omondi aliifungia Police bao muhimu katika kipindi cha kwanza na kuwapa pointi tatu, matokeo yameiondoa klabu hiyo katika eneo la kushushwa daraja.
Akizungumza baada ya mechi hiyo, Stanojavic mwenye umri wa miaka 44, alieleza kufurahishwa na mwenendo wa timu yake na kusema kuwa ushindi huo ulionyesha uwezo wa timu hiyo.
Kwa sasa Police FC wako katika nafasi ya 8 kwa pointi 8, pointi 6 nyuma ya viongozi Kakamega Homeboyz.
Imeatayarishwa na Antony Nyongesa
English 












































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































