SERIKALI YAAHIDI USALAMA UCHAGUZINI
Serikali imewahakikishia wapiga kura kwamba usalama umeimarishwa katika maeneo yote ambako uchaguzi mdogo umeratibiwa kufanyika Alhamisi wiki hii ikiwemo eneo bunge la Mbeere North ambako vurugu zimekuwa zikishuhudiwa.
Akizungumza kwenye msururu wa kampeni eneo hilo, naibu Rais Kithure Kindiki amekariri kuwa vitendo vya vurugu havitavumiliwa na serikali.
Kindiki aidha ametetea utendakazi wa serikali eneo hilo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































