#Football #Sports

UNITED WAPATA ‘JERAHA’ LA KWANZA CHINI YA CARRICK

Bao la Benjamin Sesko katika dakika ya 96 liliihakiikisha Manchester United rekodi ya kutopoteza mechi chini ya kocha mshikilizi Michael Carrick, baada ya kulazimisha sare ya bao 1-1 ugenini dhidi ya West Ham United.

Carrick alikuwa ameshinda mechi zote 4 tangu alipochukua hatamu Old Trafford, ila msururu wa ushindi mfululizo ulitiwa breki na nyundo la Wes Ham, waliochukua ushindi kupitia kwa Tomas Soucek kunako dakika ya 50.

Katika matokeo mengine, Chelsea walipoteza nafasi ya kuibandua Manchester United nje ya top 4 jana usiku, baada ya kupoteza uongozi wa mabao 2 na kuambulia sare ya mabao 2-2 dhidi ya Leeds United.

Joao Pedro aliwaweka the Blues uongozini katika dakika ya 24, kabla ya Cole Palmer kuongeza la pili kupitia mkwaju wa penalti katika dakika ya 58.

Hata hivyo, dakika 6 za utepetevu katika kipindi cha pili zilishuhudia uongozi huo ukiyeyuka kama bonge la aiskrimu juu ya moto.

Lukas Nmencha akifuta bao moja katika dakika ya 67 kupitia mkwaju wa penalti, kabla ya Noah Okafor kufunga la pili licha ya utata wa handiboli uliozingira bao hilo.

Wakati uo huo, masaibu ya Tottenham yaliongezwa na wanyonge wenzao Newcastle kwa kichapo cha mabao 2-1 nyumbani, mkufunzi Eddie Howe akionekana kuokoa kazi yake huku mwenzake wa SpursThomas Frank akiwa taabani kutokana na kichapo hicho.

Kwa sasa Chelsea wangali katika nafasi ya 5 kwa pointi 44, United wakiwa wa 4 kwa pointi 45.

Newcastle wamepanda hadi nafasi ya 10 kutokana na ushindi huo kwa pointi 36, huku Spurs wakishuka hadi nafasi ya 16 kwa pointi 29, na kazi kwao sasa ni kujiokoa kutoka kwenye hatari ya kushushwa Daraja.

Leo hii ni zamu ya Manchester City kupunguza mwanya wa pointi kati yao na Arsenal hadi pointi 3 watakapoialika Fulham leo usiku, kabla ya Arsenal kufunga safari kuelekea Brentford, ikisubiriwa kuona nani mkali kati ya Gunners na The Bees.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

UNITED WAPATA ‘JERAHA’ LA KWANZA CHINI YA CARRICK

LEOPARDS WATATOA TENA KUCHA, KOCHA AMBANI

UNITED WAPATA ‘JERAHA’ LA KWANZA CHINI YA CARRICK

SIFUNA AKOSA KIKAO CHA NEC YA ODM

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *