GACHAGUA ATAKA SERIKALI KUTANGAZA UKAME JANGA LA KITAIFA.
Kinara wa DCP Rigathi Gachagua sasa anataka serikali itangaze hali ya ukame nchini kuwa janga la kitaifa.
Akizungumza na wanahabari, Gachagua amesema eneo la kaskazini mwa Kenya lililoathirika zaidi linahitaji msaada wa dharura.
Gachagua Pia amewalaumu viongozi wa kaskazini mashariki kwa kusalia kimya, licha ya ukame kumaliza mifugo na kuathiri wakaazi wake.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 





























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































