#Athletics #Sports

DEAFLYMPICS: WAMBUI AVUNJA REKODI YA DUNIA

Mkenya Ian Wambui aliiletea nchi fahari katika mashindano ya wanariadha wasio na uwezo wa kusikia ya Tokyo 2025 Summer Deaflympics, akivunja rekodi ya dunia aliposhinda nishani ya dhahabu katika mbio za mita 5,000 kwa wanaume.

Wambui alikamilisha mbio hizo kwa muda wa dakika 13, sekunde 52.83, na kuvunja rekodi ya dakika 14, sekunde 2.90 iliyowekwa mwaka wa 2013 na mkenya mwenzake Symon Kibai.

Wakenya walitamalaki mbio hizo, James Musembi akichukua nishani ya fedha naye Nelson Kipkorir akiridhika na shaba katika mbio hizo zilizoandaliwa ugani Komazawa Olympic Park.

Wambui ambaye kwa sasa anajivunia dhahabu 2 jijini Tokyo baada ya kushinda nyingine katika mbio za mita 10,000 mapema wiki hii, amesema kuvunja rekodi kulikuwa sehemu ya mpango wake.

Awali kabla ushindi wa Wambui, Viola Jelimo aliishindia Kenya nishani ya shaba katika mbio za mita 5,000 kwa wanawake, akiandikisha muda wa dakika 17, sekunde 26.83 nyuma ya Mira da Silva wa Ureno na Mrusi Emilyevna Iuliia.

Hadi tukienda hewani, Kenya ilikuwa na jumla ya medali 14, zikiwemo dhahabu 5 sawa na fedha, na shaba 4.

Kenya ilipoteza fursa nyingine ya kupata medali zaidi baada ya Simon Menza kuanguka katika mbio za kupokezana vijiti alipogusana na mwanariadha wa Japan, ila rufaa ya Kenya ikatupiliwa mbali kwa misingi ya kiufundi.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

DEAFLYMPICS: WAMBUI AVUNJA REKODI YA DUNIA

SERIKALI YAAHIDI USALAMA UCHAGUZINI

DEAFLYMPICS: WAMBUI AVUNJA REKODI YA DUNIA

JUNIOR STARLETS ROBO FAINALI

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *