WAVINYA AONYA MAAFISA WANAOFYONZA MAFUTA YA KAUNTI
Gavana wa Machakos Wavinya Ndeti ametoa onyo kali kwa maafisa wa kaunti wanaohusishwa na uhalifu wa kufyonza na kutumia vibaya mafuta ya kaunti katika vituo vya mafuta ya petroli
Wavinya amesema tabia hiyo imekuwa ikidhoofisha utoaji wa huduma na kusababisha ufujaji mkubwa wa rasilimali za umma, jambo linalowakosesha wananchi huduma wanazostahili kutoka kwa serikali ya kaunti.
Wavinya amesisitiza kuwa hatua kali zitachukuliwa dhidi ya wote watakaopatikana na hatia, akiahidi kuwa kaunti ya Machakos haitavumilia vitendo vya ufisadi katika idara yoyote.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































