IDADI NDOGO YA WAPIGA KURA YAZUA HOFU
Tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC imeibua hofu kuhusu idadi ndogo ya wapiga kura wapya waliosajiliwa, IEBC ikiripoti kuwasajili wakenya elfu 90 pekee katika kipindi cha mwezi mmoja.
Kwa mujibu wa tume hiyo, kaunti ya Nairobi inaongoza kwa wapiga kura wapya ambao ni 16,000, huku kaunti za Tana River, Marsabit, Isiolo na Samburu zikikosa kufikisha watu 500 katika kipindi hicho.
Viongozi wa kisiasa sasa akiwemo aliyekuwa naibu Rais Rigathi Gachagua wametoa wito kwa vijana kujisajili.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































