WETANG’ULA ATAKA NCIC IVUNJILIWE MBALI
Spika wa bunge la kitaifa Moses Wetang’ula amelitaka bunge kuvunjilia mbali tume ya kitaifa kuhusu uwiano na utangamano, NCIC, kwa misingi kwamba imeshindwa kutekeleza wajibu wake.
Akirejelea matamshi ya aliyekuwa naibu rais Rigathi Gachagua dhidi ya mbunge wa Nyaribari Chache Zaheer Janda, Wetang’ula amemwagiza kiongozi wa walio wengi bungeni Kimani Ichung’wa kuhakikisha kuwa NCIC inavunjiliwa mbali iwapo haiwawajibisha wanaoeneza chuki.
Amependekeza kubuniwa kwa tume mpya.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 




























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































