WATU 11 WAMEFARIKI KUFUATIA AJALI YA NDEGE
Watu 11 wameripotiwa kufariki katika ajali ya ndege ambayo imeanguka katika eneo la tsimba-matuga eneo bunge la matuga kaunti ya Kwale.
Ajali hiyo imethibitishwa na mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya usafiri wa anga nchini emile arao akisema kwamba ndege hiyo, nambari ya usajili 5y-cca, iliyokuwa na watalii ilikuwa ikielekea kichwa tembo maasai mara kutoka diani kabla ya kuanguka mapema hii leo.
Maafisa kutoka idara ya uchunguzi wa ajali za ndege wameanzisha uchunguzi.
Imetayarishwa na Jones Koikai
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































