#Football #Sports

NYOTA YA STARLETS KWENYE MIZANI

Timu ya taifa ya wanawake ya soka Harambee Starlets imekamilisha mazoezi yake kwa matayarisho yay a mechi ya leo ya mkondo wa pili ya kufuzu mashindano ya WAFCON mwaka ujao nchini Morocco.

Starlets watakabiliana na The Gambia nchini Senegal kwenye mechi hiyo ya marudiano, wakiwa tayari wanaongoza kwa mabao 3:1 kufuatia ushindi wao wa mkondo wa kwanza, na sasa watahitaji ushindi ama sare ya aina yoyote kufuzu mashindano ya WAFCON.

Mechi hiyo itaanza saa moja jioni saa za Afrika Mashariki, na kufuzu kwao itakuwa ni historia kwa vipusa hao wa Beldine Odemba, ambao wamekuwa nje ya mashindano hayo tangu mwaka wa 2016.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

NYOTA YA STARLETS KWENYE MIZANI

META, TIKTOK KUTII SHERIA ZA MIAKA 16

NYOTA YA STARLETS KWENYE MIZANI

DROO YA CAF CONFEDERATIONS

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *