KAMPENI ZA CHAGUZI NDOGO KIKOMO
Kampeni za chaguzi ndogo katika maeneo mbali mbali ya taifa zimekamilika rasmi huku macho yote sasa yakielekezwa kwa tume ya IEBC kuona jinsi itakavyoendesha chaguzi hizo Alhamisi wiki hii, hasa kutokana na madai kwamba tume hiyo imeonyesha miegemeo ya kisiasa.
Miongoni mwa maeneo kutakakofanyika chaguzi hizo ni wadhifa wa useneta kaunti ya Baringo, maeneo bunge ya Malava, Ugunja, Kasipul, Magarini, Mbeere North na wadi ya Kabuchai.
Serikali na upinzani zinalenga kutangaza ubabe wao wa kisiasa kupitia chaguzi hizo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 

























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































