#Local News

FAMILIA ZA MKASA MALAHA ZAJIANDAA KWA MAZISHI

Familia zilizowapoteza jamaa zao kwenye mkasa wa ajali katika eneo la Malaha Junction kwenye barabara kuu ya Webuye kuelekea Kitale zimeanzisha mipango ya mazishi ya wapendwa wao, huku majonzi yakiendelea kutanda katika vijiji hasa Sipala, kilichowapoteza watu 9 usiku huo.

Waathiriwa 6 kati ya jumla ya 15 ni ndugu wa familia moja ya David Kimisu, wengine watatu kwenye Kijiji hicho wakiwa jamaa za familia hiyo ambayo imetaja vifo hivyo kuwa pigo kwao.

Mansura 16 wanaendelea kupokea matibabu hospitalini.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *