WAIGURU AZINDUA UJENZI WA KMTC
Gavana wa kirinyaga Anne Waiguru amezindua ujenzi wa chuo cha mafunzo ya matibabu nchini cha kwanza Kirinyaga, karibu na hospitali ya rufaa ya Kerugoya.
Kulingana na gavana huyo hatua hii inaonyesha ushirikiano kati ya serikali za kaunti na kitaifa.
Mradi huu unalenga kuboresha utoaji wa huduma za afya na kuwapa vijana elimu na ajira.ujenzi huo unaanza kwa jingo la ghorofa mbili na utakamilika ndani ya mwaka mmoja.
Imetayarishwa na Jones Koikai
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































