KNCHR YAPUZILIA MBALI CHAGUZI
Chaguzi ndogo zilizopita hazikuwa huru na haki kutokana na matumizi ya wahuni, hongo na maafisa wa serikali kushawishi matokeo ya chaguzi hizo.
Ndiyo kauli ya tume ya kitaifa ya kutetea haki za kibinadamu, ikisema maafisa wake walinyimwa ruhusa ya kuingia katika baadhi ya vituo vya kujumlisha kura kutoa uangalizi wao inavyohitajika kisheria.
Wameitaka IEBC kuwajibikia matukio hayo na vifo vya watu 3.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































