KINYANG’ANYIRO CHA TIKETI ZA KOMBE LA DUNIA ULAYA
Kampeni ya kuwania tiketi za moja kwa moja za kufuzu kombe la dunia kwa bara Ulaya inatamatika leo usiku kwa mechi kadhaa ambazo zimeratibiwa kusakatwa katika nyuga mbali mbali.
Ubelgiji walio na pointi 15, 2 mbele ya North Macedonia, watahitaji ushindi katika mechi yao ya mwisho dhidi ya Liechtenstein, nao North Macedonia watalenga kupata ushindi dhidi ya Wales huku wakiomba njia ya Ubelgiji iwe na utelezi.
Kwenye mechi zingine, Uhispania watavaana na Uturuki, Sweden na Slovenia, nao Kosovo wakiwaalika Uswizi.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 












































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































