MAAFISA WA KLINIKI KAUNTI YA MARSABIT WANAENDELEA NA MGOMO WAO
Maafisa wa kiliniki kutola kaunti ya Marsabit wameendelea na mgomo ambao umeingia wiki ya nne sasa.
Mgomo huo umeendelea huku mvutano ukiendelea kuhusu mkataba uliosainiwa na serikali ya kaunti ya Marsabit na muungano wa maafisa hao wa kliniki mwezi aprili mwaka huu.
Maafisa hao wa kliniki wanaitaka serikali ya kaunti sasa kuwajibika ipasavyo na kutekeleza matakwa yao.
Imetayarishwa na Jones Koikai
English 


























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































