#Football #Sports

SUPER EAGLES WASITISHA MGOMO,WAREJELEA MAZOEZI

Wachezaji wa timu ya taifa ya soka ya Nigeria Super Eagles, wamesitisha mgomo wao kuhusu malipo ya marupurupu na kurejelea mazoezi baada ya mzozo wa marupurupu hayo kuripotiwa kutatuliwa.

Super Eagles wanajiandaa kwa pambano la mwondoano dhidi ya Gabon hii leo nchini Morocco, katika kipute cha timu 4 zinazowinda tiketi ya kushiriki kombe la dunia mwaka ujao kupitia mchujo.

Nahodha wa timu hiyo William Troost-Ekong anayewajibikia klabu ya Al-Khoolod nchini Saudi Arabia, amethibitisha kupitia ukurasa wake wa mtandao wa X kwamba mzozo huo umetatuliwa, na kwamba macho yao sasa yameelekezwa kwa mechi zijazo.

Wachezaji hao walianza mgomo wao Jumanne, wakilidai shirikisho la soka nchini humu NFF marupurupu yao ya mazoezi, ya hadi mwaka 2019

Mshindi kati ya Nigeria na Gabon atapambana na mshindi kati ya DR Congo na Cameroon kwenye fainali Jumapili.

Mshindi wa fainali hizo atamenyana na timu zingine kutoka mabara mengine mapema mwaka ujao ili kusaka tiketi ya kushiriki kombe la dunia mwaka ujao nchini Marekani, Mexico na Canada.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

SUPER EAGLES WASITISHA MGOMO,WAREJELEA MAZOEZI

KPA YAWAKA MOTO WA VIKAPU

SUPER EAGLES WASITISHA MGOMO,WAREJELEA MAZOEZI

ITALIA KUKOSA KOMBE LA DUNIA KWA MARA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *