#Local News

KENYA KWANZA, DAP-K ZAVAANA MALAVA

Mirengo pinzani ya kisiasa katika eneo bunge la Malava kaunti ya Kakamega imeimarisha kampeni kwa wagombeaji wao katika uchaguzi mdogo eneo hilo, huku mrengo unaomuunga mkono mgombeaji wa chama cha DAP-K Seth Panyako ukiibua madai ya njama ya kuvuruga uchaguzi huo.

Ukiongozwa na seneta wa kaunti hiyo Boni Khalwale na naibu kinara wa DAP-K George Natembeya, mrengo huo umewataka wafuasi hao kuwa watulivu na imara wanapoelekea kwenye uchaguzi huo wa tarehe 27.

Hata hivyo, mrengo wa Kenya Kwanza ukiongozwa na spika wa seneti Amason Kingi, umepuzilia mbali madai hayo.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

KENYA KWANZA, DAP-K ZAVAANA MALAVA

UPINZANI WAMLIKA IEBC MBEERE NORTH

KENYA KWANZA, DAP-K ZAVAANA MALAVA

WAATHIRIWA CHESONGOCH WASALIA KAMBINI

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *