OMTATAH APINGA MKATABA WA KENYA-MAREKANI KORTINI
Shutuma dhidi ya mkataba wa ushirikiano katika sekta ya afya uliotiwa Saini kati ya Kenya na Marekani umechukua mkondo mpya, seneta wa Busia Okiya Omtatah sasa akielekea mahakamani kuzuia utekelezwaji wake.
Kwenye kesi yake, Omtatah amesema mkataba wa huo wa shilingi bilioni 208 za Kenya unaoiwezesha Marekani kuwekeza moja kwa moja katika taasisi za afya kwa kipindi cha miaka 5, uliafikiwa bila kujumuisha maoni ya wananchi inavyohitajika kisheria, akihofia kuwa huenda fedha zikafujwa bila uwajibikaji.
Haya yanajiri huku wadau akiwemo mwanasheria PLO Lumumba na mtaalam wa mawasiliano Barrack Muluka wakitilia shaka makubaliano hayo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 




















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































