#Local News

ASANTE KWA MAAFANDE

Awamu ya mwisho ya nyongeza ya mishahara ya maafisa wa polisi, wale wa magereza na maafisa wa idara ya huduma ya kitaifa ya vijana, NYS, itatekelezwa Julai mwaka huu ikiwa ni sehemu ya mpango wa kutekeleza mageuzi katika sekta ya usalama nchini.

Kupitia taarifa, katibu katika wizara ya usalama wa kitaifa Raymond Omollo, amesema uamuzi huo unafuatia mkutano wa kamati ya kitaifa kuhusu utekelezaji wa mageuzi hayo, akisema nyongeza ya mishahara kwa miaka 3 mfululizo kwa maafisa hao ni ya juu zaidi tangu taifa lipate uhuru.

Kwenye nyongeza hiyo, afisa wa polisi wa ngazi ya juu katika cheo cha konstebo, atapokea mshahara wa shilingi 57,700, kutoka shilingi 38,975 za sasa, huku yule anayefuzu akianza na mshahara wa shilingi 29,296, kutoka 20,390 za sasa.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

ASANTE KWA MAAFANDE

ROONEY ONYANGO APATA AFUENI

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *