NDAKWA AIBUKA MSHINDI MALAVA
Tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC imemtangaza David Ndakwa wa UDA kama mshindi katika kinyang’anyiro cha ubunge eneo bunge la Malava, na kumbwaga mshindani wake wa karibu Seth Panyako wa DAP-K.
Kwa mujibu wa IEBC, Ndakwa amepata jumla ya kura 21,564 huku Panyako akifuata kwa karibu na kura 20,210 kwenye kinyang’anyiro kilichokumbwa na vurugu na uharibifu wa mali.
Wilberforce Indai wa Kenya Moja amemaliza wa 3 na kura 626, jumla ya kura 43,675 pekee zikipigwa kati ya wapiga kura 94,417 waliosajiliwa.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 












































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































