SERIKALI KUIMARISHA USHIRIKIANO NA CHINA KUBORESHA MIUNDOMBINU
Rais William Ruto amesema serikali yake itaendelea kuimarisha ushirikiano na China katika hali ya ushirikiano na maendeleo ya pamoja.Ruto, ambaye alikuwa mwenyeji wa ujumbe kutoka Benki ya Exim-Import ya China (China Exim Bank) ukiongozwa na Mwenyekiti Chen Huaiyu jijini Nairobi, amesema kuongezeka kwa uwepo wa kampuni za Kichina nchini Kenya kunaonyesha imani yao katika utulivu wa nchi na utayari wa taifa hilo wa kupanua uwekezaji.
Kwa upande wake Chen amesisitiza dhamira dhabiti ya benki hiyo ya kuimarisha ushirikiano na Kenya, akibainisha nia ya kuendelea ya China katika kukuza uhusiano wa kiuchumi na kibiashara ambao unaleta manufaa madhubuti kwa watu wa Kenya.Chen amesema kuwa benki hiyo inachukulia Kenya kama mshirika wa kimkakati na iko tayari kusaidia miradi inayoboresha muungano, kuchochea uwekezaji na kuendeleza maendeleo endelevu ya kiuchumi.
Vile vile ameonyesha imani kuwa mradi wa Mfumo wa Usafiri(ITS) utaimarisha zaidi ushirikiano baina ya nchi hizo mbili na kuchangia pakubwa katika ajenda ya maendeleo ya muda mrefu ya Kenya.Makubaliano hayo yalitiwa saini na Waziri wa hazina ya kitaifa John Mbadi na Zhu Jia, naibu meneja mkuu wa Idara ya Biashara Kuu katika Benki ya Exim ya China.
Imetayarishwa na Maurine Amwayi
English 












































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































