#Football #Sports

KOCHA WA SHABANA FC AJIUNGA NA TIMU YA TAIFA YA U-17

Kocha mkuu wa Shabana FC, Peter Okidi, ameonyesha imani kamili
kwa msaidizi wake Bernard Mwalala, atakayesimamia timu hiyo
wakati yeye akiungana na timu ya taifa ya wanafunzi wa chini ya
miaka 17, Junior Stars, kwa mashindano ya kufuzu AFCON U17 mwaka
2026 yatakayofanyika nchini Ethiopia.
Okidi atahudumu kama kocha msaidizi wa William Muluya wa
Kariobangi Sharks katika mashindano hayo ya kanda yatakayoanza
Novemba 15 na kuhitimishwa Desemba 2 mjini Addis Ababa.
Wakati huo, Mwalala atakuwa akisimamia majukumu ya Shabana FC,
kuanzia mechi ya nyumbani dhidi ya Nairobi United katika Uwanja wa
Gusii, kisha michezo ya ugenini dhidi ya Murang’a Seal na Kenya
Police FC.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *