#Football #Sports

RODRI APIGWA FAINI, APONEA MARUFUKU

Kiungo wa Manchester City na mshindi wa Ballon d’Or, Rodri, ametozwa faini ya pauni 80,000, sawa na takribani shilingi milioni 13.8 za Kenya kuhusiana na kauli zake alizitoa dhidi ya refa aliyesimamia mehi kati ya City na Tottenham mwezi jana.

Kwenye kauli hizo, Mhispania huyo alikosoa hatua ya refa kuruhusu bao la Dominic Solanke, Rodri akiamini kuwa Solanke alimbwatua beki wa City Marc Guehi kabla ya kufunga bao hilo, mechi hiyo ikiishia kwenye sare ya mabao 2-2.

Akizungumza baada ya mechi hiyo, Rodri alitoa mifano zaidi ya marefa kutoa maamuzi anayoamini yasiyofaa dhidi ya City, ikiwemo katika mechi dhidi yao na Manchester United ambapo Diogo Dalot hakuonyeshwa kadi nyekunu baada ya kumcheea visivyo Jeremy Doku.

Kulingana naye, maamuzi mengi yamekuwa dhidi yao baada yao kushinda mataji mengi, akisema hatua hiyo si sawa.

Hata hivyo, afueni yake ni kwamba tume ya shirikishi la soka nchini Uingereza, FA, haikupiga marufuku ya mechi yoyote baada ya kupatikana na hatia ya kuwakosoa marefa.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *