#Football #Sports

JUNIOR STARS WAZIMWA NA TANZANIA

Timu ya taifa ya Tanzania na Uganda Cubs kwa wachezaji wasiozidi umri wa miaka 17 zimefuzu dimba la AFCON U17 litakaloandaliwa nchini Morocco mwaka ujao.

Tanzania ilipata tiketi ya kuwakilisha ukanda wa CECAFA kwenye mashindano hayo baada ya kuizima Junior Stars ya Kenya kwa mabao 3-1 nchini Ethiopia.

Kwa upande wao, Uganda Cubs waliwabandua wenyeji Ethiopia kwa kichapo cha mabao 3-0, na kujikatia tiketi yake.

Kenya na Ethiopia zitawania nafasi ya 3 katika juhudi za kuokoa azma yao ya kufuzu dimba la AFCON U17.

Mechi hiyo itachezwa hapo kesho kabla ya mabingwa wa mwaka 2024 Uganda kumenyana na Tanzania kwenye fainali.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

JUNIOR STARS WAZIMWA NA TANZANIA

MATUMAINI YA NAIBOIS CAF YAFIFIA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *