#Football #Sports

GUEYE ASEMA SENEGAL ILITUMIA HASIRA KUSHINDA AFCON

Mfungaji wa bao la ushindi katika fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika, Pape Gueye, amesema Senegal ilichochewa na hali ya kutotendewa haki baada ya Morocco kupewa penalti ya utata iliyokaribia kuwagharimu taji hilo.

Mchezo huo uliochezwa katika uwanja wa Prince Moulay Abdellah mjini Rabat ulikuwa bado bila bao hadi dakika za mwisho za muda wa majeruhi, wakati Morocco walipopewa mkwaju wa penalti kufuatia marejeo ya VAR baada ya Brahim Diaz kuangushwa ndani ya eneo la hatari.

Senegal walikuwa tayari wamekasirishwa baada ya bao lao kukataliwa dakika chache awali kwa madai ya faulo nyepesi, hali iliyozua hasira kubwa huku baadhi ya wachezaji wao wakiondoka uwanjani kwa ishara ya kupinga uamuzi huo.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *