#Business

NAFASI NYINGI MPYA ZA AJIRA NI ZA KSH50,000–KSH100,000 – KNBS

Kampuni na taasisi za umma zilianzisha kazi rasmi za ziada 206,617 kwa Wakenya wanaopata kati ya Ksh50,000 na Ksh100,000 kwa mwezi katika kipindi cha miaka mitano hadi 2024, na kufanya hii kuwa bendi ya malipo inayokuwa kwa kasi zaidi, kufuatia data kutoka Ofisi ya Kitaifa ya Takwimu ya Kenya (KNBS).

Wafanyikazi katika kitengo hicho cha mishahara walichangia 43.8% ya kazi rasmi 471,191 zilizoundwa katika kipindi hicho. Idadi yao jumla iliongezeka kutoka milioni 1.25 mwaka 2020 hadi milioni 1.46 mwaka jana, ikiwa ni ongezeko la 16.5%.

Kundi hilo sasa linaunda asilimia 45.5 ya wafanyakazi rasmi wa Kenya milioni 3.2, wakifuatiwa na wafanyakazi wanaopata Ksh30,000 hadi Ksh49,999, ambao ni asilimia 32.2. Kampuni Za kibinafsi ZIlizalisha 69.1% ya kazi mpya katika mabano ya Ksh50,000 hadi Ksh99,999, na zingine zikitoka kwa sekta ya umma.

Kama ilivyoripotiwa, wafanyakazi wengi katika kundi hilo wameajiriwa katika elimu, utawala wa umma na ulinzi, viwanda, kilimo, na biashara, ikiwa ni pamoja na wataalamu kama vile walimu, maafisa wa kijeshi, wauzaji wa benki na wafanyakazi wa utawala.

Data ya KNBS pia inaonyesha ukuaji wa kasi miongoni mwa watu wa kipato cha chini, huku wafanyikazi wanaopata chini ya Ksh30,000 wakipanda kwa 33.4%, ikionyesha changamoto katika kuunda kazi zenye malipo mengi huku kukiwa na ushuru wa juu na shinikizo la baada ya janga.

Imetayarishwa na Maurine Amwayi

NAFASI NYINGI MPYA ZA AJIRA NI ZA KSH50,000–KSH100,000 – KNBS

CITY KUPUNGUZA MWANYA NA ARSENAL

NAFASI NYINGI MPYA ZA AJIRA NI ZA KSH50,000–KSH100,000 – KNBS

UPINZANI WADAI KUIBIWA CHAGUZI NDOGO

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *