#Boxing #Sports

ZARIKA ‘KUMSHUSHA BEI’ VUNJABEI KWENYE FEATHERWEIGHT

Bingwa wa zamani wa pigano la WBC Super bantamweight Fatuma Zarika ameratibiwa kudhihirisha ni kwanini akapewa jina la Mkono chuma ama Iron Fist atakapomenya na Mtanzania Halima Vunjabei katika pigano la Super Featherweight katika jumba la Masshouse eneo la Ngong Racecourse hii leo.

Pigano hilo ambalo limeandaliwa kupitia ushirikiano wa tume ya wanamasumbwi nchini KPBC, inaashiria kufufuliwa kwa mchezo wa masumbwi, likijumuisha tajriba na chipukizi.

Zarika anarejea ulingoni baada ya takribani mwaka mmoja, analenga kuongeza ushindi kwenye rekodi yake ya kushinda mapigano mara 34 na kupoteza mara 14 baada ya mapigano 50 ya taaluma yake.

Kwa upande wa wanaume, Rayton Okwiri atamenyana na Mganda Muhammad Sebyala katika pigano lenye raundi 8 la Middleweight.

Okwiri, anayerejea kwa mara ya kwanza tangu Septemba mwaka jana nchini Mauritius, anajivunia ushindi mara 11 na kupoteza mara 1 pekee na atalenga kuendeleza rekodi yake ya ushindi.

Wakati uo huo, Joshua Wasike, aliyepoteza mara ya kwanza katika mapigano 5, atakabliana na Mtanzania Shabai Kaoneka katika pambano la Heavyweight.

Mwenyekiti wa tume ya KPBC Reuben Ndolo, aliyechaguliwa tena maajuzi kama Rais wa Commonwealth Boxing Council, ameeleza kujitolea kwake katika ukuzaji wa mchezo wa masumbwi.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

ZARIKA ‘KUMSHUSHA BEI’ VUNJABEI KWENYE FEATHERWEIGHT

UBABE WA HANDIBOLI WATARAJIWA WIKENDI

ZARIKA ‘KUMSHUSHA BEI’ VUNJABEI KWENYE FEATHERWEIGHT

DROO YA UEFA KUELEKEA KOMBE LA DUNIA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *