JUNIOR STARLETS ROBO FAINALI
Timu ya taifa ya soka kwa vijana wasiozidi umri wa miaka 17 Junior Stars wameweka guu moja ndani ya semifainali ya kipute cha kufuzu dimba la mataifa bingwa barani Afrika AFCON U17 mkondo wa CECAFA baada ya kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya South Sudan ugani Abebe Bikila nchini Ethiopia.
Derrick Wanyonyi alianzisha ufungaji wa mabao dakika ya 12 kabla ya Trevor Nassasiro kuongeza la pili dakika ya 89, huu ukiwa ushindi wa pili na sare moja kwa Junior Stars katika Group A.
Kutokana na matokeo hayo, Kenya na Ethiopia zinaongoza kundi hilo kwa pointi 7, wawili hao wanapojiandaa kutifua kivumbi Alhamisi wiki hii kuwania nafasi katika semifainali.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 












































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































