BUNGE, SENETI KUJADILI HOTUBA YA RAIS
Wabunge na maseneta wameratibiwa kujadili hotuba ya rais William Ruto kuhusu hali ya taifa aliyotoa wiki jana, hii ikiwa ni siku ya pili baada ya vikao hivyo kuanza hapo jana.
Kiongozi wa walio wengi katika bunge la kitaifa Kimani Ichung’wa, ametetea hotuba hiyo, akisema inaambatana na utendakazi wa serikali ya Kenya Kwanza kwa muda wa miaka 3 mamlakani.
Kwa mujibu wake, hotuba hiyo iliashiria mwelekeo sahihi wa taifa.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































