#Local News

WAKAZI WA KAPSABET WAOMBA UPANUZI WA BARABARA

Serikali imetakiwa kuchukua hatuza haraka na kupanua barabara kuu ya Kapsabet kaunti ya Nandi kuelekea Chavakali kaunti ya Vihiga, ili kuzuia visa vya ajali vinavyohusishwa na hali mbovu ya barabara hiyo.

Wakizungumza mjini Kapsabet, wakazi, madereva na wahudumu wa boda boda wamelalamikia madai ya barabara hiyo kutelekezwa na idara husika, wakisema ni nyembamba mbali na kukosa sehemu ya wanaotembea kwa miguu.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *