KENHA YAZUNGUMZIA MPANGO WA UPANUZI WA BARABARA YA KIAMBU
Kuunganishwa kwa barabara ya Muthaiga –Kiambu– Ndumberi yenye urefu wa kilomita 23.5 kunatazamiwa kupunguza msongamano wa magari kati ya kaunti za Nairobi na Kiambu.
Kulingana na taarifa iliyotolewa hapo jana na KENHA ni kuwa mradi huo unatarajiwa kuongeza upana wa barabara hiyo jambo ambalo pia litawakikishia wapita njia usalama wao barabarani.
Mamlaka ya Kitaifa ya Barabara Kuu ya Kenya ( KeNHA ), limesema kuwa barabara hiyo itajumuisha barabara za njia 2 pande zote pamoja na njia za abiria .
Imetayarishwa na Jones Koikai
English 







































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































