#Football #Sports

HAMNA SHINIKIZO KWA NAIBOIS, MUYOTI

Kocha mkuu wa Nairobi United Nicolas Muyoti ameelezea matumaini ya timu yake kumaliza miongoni mwa 5 bora msimu huu wa kwanza katika ligi kuu nchini, akisema hawana shinikizo za kupigania taji hilo msimu huu.

Muyoti ambaye awali alikuwa kocha mkuu wa City Stars na Kakamega Homeboyz, amesema klabu hiyo itaanza kuangazia kutwaa taji hilo baada ya kujifanyia tathmini.

Naibois kwa sasa wamo katika nafasi ya 10 na pointi 12 baada ya mechi 6, pointi 7 nyuma ya viongozi Gor Mahia ambao wamesakata mechi 9.

Klabu hiyo ndiyo timu ya pekee ya Kenya ambayo imesalia katika mashindano ya mashirikisho ya bara, baada ya Police FC kubanduliwa nje ya kipute cha klabu bingwa barani Afrika.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

HAMNA SHINIKIZO KWA NAIBOIS, MUYOTI

KPA MACHO SASA WBLA

HAMNA SHINIKIZO KWA NAIBOIS, MUYOTI

CITY KUPUNGUZA MWANYA NA ARSENAL

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *